Katika picha hii ya kutoka maktaba inamuonesha Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsalimia Mama Jitto Ram mara baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wa hadhara wakati wa kampeni katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mama Jitto Ram amefariki dunia mjini Morogoro baada ya kuugua ugonjwa wa moyo. Mama Jitto Ram alikuwa mbunge wa viti maalum CCM. Alikuwa mkufunzi wa manesi Muhimbili. Alikuwa mtetezi wa haki za WAVIU/PLHIV. Alikuwa mwana harakati wa kutokomeza unyanyapaa dhidi ya WAVIU/PLHIV. Khitma ya arobaini ya Mama Jitto itafanyika nyumbani kwa mwanae Morogoro, January 28, 2017 Insha Allah. Inna lillahi wa inna ilaihi raajiun. Amen
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...