Na Adili Mhina
Katika kuitikia na kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli la Serikali kuhamia Dodoma, Tume ya Mipango inatarajia kuanza kuhamisha watumishi wake kuelekea Makau Makuu ya Nchi ifikapo mwezi Machi Mwaka huu. 
Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alipokutana na watumishi wa taasisi hiyo Ijumaa Januari 26, 2017 kwa lengo la kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu taasisi hiyo.
Pamoja na agenda zingine kujadiliwa katika kikao hicho, suala la kuhamia Dodoma lilionekana kuchukua nafasi kubwa miongoni mwa wafanyakazi mara baada ya ratiba ya zoezi hilo kutolewa rasmi ambapo wengi walionesha kufurahishwa na kutendo cha kutimiza ahadi ya Rais kwa wananchi ya kuhamia Dodoma.
Mwanri alieleza kuwa Tume ya mipango itahamisha watumishi wake katika awamu tatu ambapo makundi mawili yanatarajiwa kuhamia Dodoma ndani ya mwaka huu.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri Akiongea na watumisi wa Tume ya Mipango (hawapo pichani) wakati wa mkutano wake na watumishi hao. Kulia ni Naibu Katibu Mtendaji anayesimamia Klasta ya Sekta za Uzalishaji Bw. Maduka Kessy na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bw. Abdulrahman Mdimu akifuatiwa Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...