Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (CAF) limetoa nafasi ya mwisho kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Jamhuri ya Congo
(FECOFOOT) kumpeleka mchezaji Langa Lesse Bercy (pichani) jijini Libreville, Gabon kwa
ajili ya kipimo kipya cha MRI ili kutambua umri wake.
CAF limetaka FECOFOOT kumpeleka mchezaji huyo huko Libreville,
Gabon ndani ya siku 10 zijazo kuanzia jana Januari 12, 2017.CAF limepata kumwita mchezaji huyo mara mbili mwaka jana, na
FECOFOOT imeshindwa kumpeleka kwa sababu mbalimbali wanazozijua FECOFOOT.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano ya kimataifa ya vijana wenye
umri wa chini ya miaka 17, vijana waliohitajika kucheza ni wale wenye umri wa
chini ya miaka 17.
Langa Lesse Bercy, amelalamikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kwamba amezidi umri hivyo kuhitajika kumpeleka kwani hakustahili
kucheza hatua ya kufuzu kwa michuano hiyo ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa
vijana.
Fainali za vijana zinatarajiwa kufanyika katika nchi nyingine
itakayotangazwa hapo baadaye baada ya Madagascar kuondolewa kuandaa fainali
hizo baada ya kubainika kutokamilisha baadhi ya taratibu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...