Baraza la Mtihani la Taifa, (Necta) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha pili, ambapo wanafunzi 372,228 (kati ya 435,075) wamefaulu sawa na asilimia 91.02.Kiwango hicho cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 2 ikilinganishwa na asilimia 89.12 ya wanafunzi waliofaulu mtihani huo mwaka jana.
Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk Charles Msonde alisema jumla ya wanafunzi 435,075 walioandikishwa kufanya mtihani huo kati yao wasichana ni 189,161 na wavulana ni 183,067.
Dk Msonde alisema ufaulu umeongezeka mwaka huu katika masomo ya msingi na wanafunzi wamefanya vizuri zaidi kwenye somo la kiswahili.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk Charles Msonde amesema jumla ya wanafunzi 435,075 walioandikishwa kufanya mtihani huo kati yao wasichana ni 189,161 na wavulana ni 183,067.
KUTAZAMA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI BONYEZA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...