Shirika
la Umoja wa Mataifa nchini limeadhimisha Siku ya Kimataifa ya
Kuwakumbuka Wahanga wa Maangamizi Makuu ya Moto dhidi ya Wayahudi kwa
kuwakutanisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Dar es Salaam na
kuwapa elimu kuhusu maangamizi hayo.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo alisema ni jambo jema kwa wanafunzi hao kupata elimu kuhusu maangamizi ambayo yalifanywa na kiongozi wa zamani wa Ujerumani, Adolf Hitler kwani hata wao wanaweza kuja kuwa viongozi kwa miaka ijayo hivyo kama watapatiwa elimu mapema watajifunza ni mambo gani kiongozi anapaswa kufanya na yapi hapaswi kwa faida ya kila mmoja.
“Kwa nyie kama wanafunzi ambao kwa miaka ya baadae wengine mtakuwa viongozi mnapaswa kujifunza kwa jambo kama hili ambalo alifanya Hitler kuwa sio jambo jema, kila binadamu ana haki sawa hakuna ambaye anamshinda mwenzake na huo ndiyo msimamo wa Umoja wa Mataifa,” alisema Vuzo.

Aidha
Afisa Habari huyo alizungumza kuhusu siku mauaji ambayo yalifanywa na
Hitler wakati akiwa kiongozi wa Ujerumani katika kipindi cha mwaka 1933
hadi 1939, “Alikuwa akichagua watu ambao wanaonekana kuwa tofauti na
kuwaondoa katika jamii ya Wajerumani, anawapeleka katika kambi maalumu
na anawaua wengine wanawekwa katika kambi maalumu wanafanyishwa kazi
ngumu bila malipo na waliokuwa wanashindwa na wao wanauawa kwa kuchomwa
moto hadi kufa,
Vuzo aliongeza kwa kusema kuwa, “Mauaji ya moto ni mauaji hatari kuwahi kutokea duniani, ilikuwa ni dhana ya Adolf Hitler kutaka Wanazi kuwa ni watu ambao wamenyoka lakini kumbe ilitakiwa aishi na watu wote katika jamii lakini alipinga hilo,” “Lakini pia alikuwa hawapendi Wayahudi, walikuwa wafanyabiashara wazuri lakini yeye aliwapinga na hata akawa anawambia wananchi wake kuwa Wayahudi kuwa hawafai katika jamii na wasinunue kitu chochote kutoka kwao.”

Kwa
upande wa Afisa Habari wa Ubalozi wa Ujerumani nchini, Susann Keller
alisema kitendo ambacho kilifanywa na Hitler hakikubaliki na ni jambo
ambalo Wajerumani wamekuwa wakijutia kila muda kutokana na vitendo vya
kikatili ambavyo vilifanyika vilivyosababisha watu wanaokadiriwa kufikia
milioni 55 na kati yao milioni sita wakiwa ni Wayahudi kupoteza maisha.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Elimu kwa ajili ya maisha
Bora ya Baadae.” .
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...