Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na mtoto mwenye ulemavu wa ngozi katika shule ya msingi Miembeni
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akimkabidhi mifuko mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa shule ya miembeni, Kuruthumu Hamisi
Picha ya pamoja na ya Naibu Meya na wazazi wa wanafunzi wanaosoma Miembeni shule ya msingi
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akimkabidhi mifuko mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa shule ya miembeni, Kuruthumu Hamisi
Na Humphrey
Shao, Globu ya Jamii.
Katika
kutekeleza sera ya elimu bure Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa
Vingunguti , Omary Kumbilamoto amekabidhi mifuko 12 ya Saruji kwa ajili ya
ujenzi wa shule ya msingi Miembeni.
Kumbilamoto
amesema kuwa mifuko hiyo ya saruji ni kwa ajili ya ujenzi wa sakafu ya madarasa mawili ambayo yamekamilika
lakini yalikuwa ayana sakafu.
“mimi
nilipita hapa nikafanya ziara na kujionea mapungufu yaliyopo katika ujenzi wa
madarasa haya ambayo yalianza kujengwa na kamati ya maendeleo ya shule kwa
kushirikiana na wananchi hivyo nimeona nichangie hii mifuko 12 ya Saruji”
Kumbilamoto amewashukuru
wananchi waliofika katika hafla hiyo kwani wameweza kujichangisha na kupata shilingi laki mojana ishirini
ambazo zitaweza kununulia mchanga wa kujengea.Ametoa wito
kwa wadau wengine wa maendeleo kuendelea kumuunga mkono Rais Magufuli kwa
kuweza kusaidia maendeleo ya elimu katika kata ya vingunguti.
Kwa upande
wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Hidaya Hamisi amemshukuru Naibu meya kwa msaada
huo ambao utaweza kusaidia kukamilika kwa ujenzi wa madarasa hayo na kuondoa
msongamano kwa wanafunzi.
Naibu
meya wa Manispaa wa Ilala, Omary Kumbilamoto akikabidhi mifuko ya
saruji kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Miembeni, Hidaya HamisiPicha ya pamoja na ya Naibu Meya na wazazi wa wanafunzi wanaosoma Miembeni shule ya msingi




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...