Usiku wa December 31, 2016 kuamkia leo mwaka mpya January 1, 2017 wanamitindo mbalimbali walikutana na kusherekea kwa pamoja Usiku wa Khanga yaani “Khanga Party”. Tukio hili kama lilivyokuwa limetaarifiwa awali limefanyika Regency Park Hotel Mikocheni jijini Dar es salaam . Mitindo mbalimbali ya vazi la Khanga kutoka kwa wanamitindo ilioneshwa kwenye stage na kuzikonga nyoyo za wahudhuriaji usiku huo.
Hafla hii iliandaliwa na Mama wa Mtindo maarufu Asya Idarous Khamsin, ambapo mbali na burudani zilizo kuwepo pia kulikuwa na Red Carpet yenye sifa kubwa ya kuwakutanisha mastaa na mashabiki wao kuweza kupiga picha za pamoja kwa ajili ya kumbukumbu. Tunawatakia mwendelezo mwema na wenye baraka wadau na wanamitindo wote wa Tanzania. (Cheers 2017)
Mama wa Mtindo Asya Idarous Khamsin akiwa katika red carpet na baadhi ya waalikwa kwenye hafla hiyo
Mama wa Mtindo Asya Idarous Khamsin akiwa katika red carpet na baadhi ya waalikwa kwenye hafla hiyo
Mamodo kwenye catwalk.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...