Na Stella
Kalinga, Simiyu.
Serikali
Mkoani Simiyu imewashauri wakulima wote
wilayani Busega wenye mashamba yaliyo
karibu na ziwa Victoria kuorodhesha jumla ya ekari za mashamba waliyonayo ili
waweze kusajiliwa na kuingizwa katika mpango wa kilimo cha umwagiliaji kinachotarajiwa kuanza mapema mwaka huu.
Ushauri
huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka katika ziara yake maalum
ya kuwatembelea wananchi wa vijiji vilivyopo kandokando ya ziwa Victoria Wilayani Busega, ambapo
ameanza na vijiji vya Nyamikoma na Nyakaboja kata ya Kabita.
Mtaka
alisema endapo wakulima watakuwa tayari kufanya kilimo cha umwagiliaji kwa kufuata ushauri wa
kitaalamu na kutumia mbegu bora watapata mazao mengi yatakayokubalika katika
soko la ndani na nje ya Mkoa ikiwa sambamba na na kujikwamua kiuchumi.
Alieleza
kuwa lengo la serikali ya Mkoa ni kuhakikisha
dhana ya mapinduzi ya kilimo kwa mfumo wa umwagiliaji inatekelezwa kwa vitendo
kwa kuwapatia elimu ya kitaalamu wakulima ili waweze kuzalisha mazao bora na
mengi yanayotosheleza soko la ndani ya nchi na kupunguza uagiziaji mazao nje ya
Mkoa.
“Tumekuja kama mkoa kuzungumza na wananchi ili wale watakaokuwa
tayari waanze kutekeleza. Ni lazima tufanye maamuzi ya kufanya mapinduzi ya
kilimo kama watu tulio kandokando ya ziwa Victoria ili uwepo ziwa utunufaishe”
amesema Mtaka.
Aidha
alifafanua kuwa kilimo hicho katika maeneo ya Wilaya ya Busega kitahusisha mazao ya Mpunga,
mboga mboga, mahindi na mazao jamii ya mikunde, hivyo wakulima kwa
kushirikiana na Serikali wanatakiwa kuendelea kubuni mbinu mbalimbali za uzalilishaji mazao hayo kwa wingi ili kwenda
sambamba na fursa ya masoko ya ndani na nje ya nchi hasa kwa mazao ya mikunde.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nyakaboja wilayani Busega katika Mkutano wa hadhara kwa lengo la kuwahamasisha kuanza kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiiaji wilayani humo.
Mkuu wa Wilaya ya Busega Tano Mwera akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Nyakaboja wilayani humo katika Mkutano wa hadhara kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kuanza kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiiaji wilayani humo.
Afisa Ardhi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Bibi.Grace Mgombera akitoa ufafanuzi wa juu masuala ya ardhi yaliyowasilishwa na wananchi wa Kijiji cha Nyamikoma B wilayani Busega kama kero kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka katika mkutano wa hadhara uliofanyik kjijini hapo.
Diwani wa Kata ya Kabita wilayani Busega akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Nyakaboja wilayani humo katika Mkutano wa hadhara kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kuanza kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiiaji wilayani humo.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Nyamikoma B Kata ya Kabita, wilayani Busega wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka katika Mkutano wa hadhara kuwahamasisha kuingia na kuanza kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiiaji wilayani humo.
Baadhi ya Maafisa wa Sekretarieti ya Mkoa walioambatana na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka katika ziara yake ya kuwahamasisha wananchi wa Busega kutekeleza mpango wa kilimo cha umwagiliaji.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...