Na Nteghenjwa Hossea, Arusha
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Arusha wameagizwa kusimamia
Halmashauri zao kujibu hoja zote zilizowasilishwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha
2015/2016 kabla ya kufika mwisho wa juma lijalo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati wa Kikao cha maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2017/2018
na mapitio ya bajeti ya nusu mwaka wa Fedha 2016/2017 kilichohusisha Halmashauri
zote za Mkoa wa Arusha na wataalam toka
Ofisi ya Mkaguzi wa hesabu za Serikali.
Akitoa Agizo hilo Mhe. Gambo alisema “Nataka kila Halmashauri
ikamilishe ujibuji wa Hoja kwa wakati na kwa majibu sahihi sio kufanya majibu
ambayo yanaibua hoja zaidi au hayajitoshelezi na kwa Halmashauri ambayo ilipata
Hati Chafu au Hati ya Mashaka kwa mwaka uliopita ianishe wataalamu waliopelekea
Halmashauri kupata Hati hizo ili waweze kuchukuliwa hatua Stahiki”.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza
kulia) akizungumza katika kikao cha maandalizi ya Bajeti 2017/2017 na mapitio
ya Bajeti 2015/2016.
Baadhi
ya Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Arusha pamoja na wadau wengine wakifuatilia Kikao
cha maandalizi na mapitio ya Bajeti.
Katibu
Tawala Msaidizi huduma za Mipango Mkoa
wa Arusha Bi. Grace Mbaruku
akiwasilisha mpango wa bajeti ya 2017/2018.
Katibu
Tawala Msaidizi Serikali za Mitaa Bi.
Susane Mnafe akiwasilisha taarifa ya changamoto za usimamizi wa Halmashauri
za Mkoa wa Arusha
1.
Viongozi
wa Mkoa na Wilaya ya Arusha wakifuatilia mawasilisho ya mpango wa Bajeti ya
mwaka 2017/2018. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...