Askari wa Usalama barabarani jijini Dar es salaam leo wamekamata gari aina ya NOAH ikiwa imebeba watoto 34 pamoja na mwalimu wao na kufanya jumla ya watu 35 katika gari Wanafunzi hao ni wa darasa la kwanza na pili kutoka shule za Diamond, Olympio, Kisutu, Maktaba na Bunge. Gari hiyo imekamatiwa eneo la mzunguko wa Gerezani likielekea Vijibweni-Kigamboni.Dereva na wahusika wa gari hiyo wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.
Home
Unlabelled
wanafunzi 34 na mwalimu mmoja katika gari aina ya Noah jijini Dar es salaam leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kwanza wazazi wa hawa watoto wanajua kwamba watoto wao wanasafiri hivi kwenda shule? Kama wanajua ningependa kujua maoni yao. Huu ni uzembe wa hali ya juu, hapa yakitokea ya kutokea watasema ni mpango wa Mungu. Smh.
ReplyDeleteWatanzania ifike mahali akili zetu ziamke tuache kusubiri serikali kutufanyia kila kitu na kumsingizia Mungu kwa kila jambo hata kwa yale ambayo tungeweza kuzuia. Mwalimu, dereva, shule na wazazi wachukuliwe hatua kali.