SERIKALI imeridhishwa na utekelezaji wa sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi na kuiagiza Bodi mpya ya Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kufanya kazi karibu na watendaji baraza hilo ili kufikia malengo yake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bi.Jennista Mhagama, amesema serikali ina imani kubwa na bodi mpya ya Baraza na hivyo kulitaka kutekeza majukumu yake kwa uwazi na ufanisi.
“Jukumu lenu kubwa ni kushauri na kuelekeza utendaji wa majukumu ya Sekretarieti ya Baraza ili waweze kuchochea Uwezeshaji unaotekelezwa na taasisi za umma na zile zile za binafsi,”alisema Bi.Mhagama wakati akizindua Bodi mpya ya Baraza juzi jijini Dar es Salaam.
Waziri Mhagama alisema kuwa Serikali inaimani kubwa Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Baraza na pasipo shaka uzoefu wenu katika masuala mbalimbali ya Uwezeshaji yataiwezesha Serikali kufikia ndoto yake ya kuona Mwananchi amewezeshwa katika maeneo yote muhimu hasa katika uchumi.
”Dhana nzima ya Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004 ni kuona kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa Tanzania inamilikiwa na watanzania wenyewe,” alisema na kuongeza kuwa jukumu la bodi ni kuhakikisha nafasi kubwa ya uwezeshaji inatolewa kwa makundi yote hasa yale yenye uwezo mdogo na kuwapa nafasi zaidi wanyonge.
Alisema yote haya yanawezekana tukishirikiana kwa pamoja katika kutekeleza azma ya serikali ya kukuza uchumi imara kwa wananchi unaoweza kuhimili ushindani katika soko la dunia katika mazingira ya utandawazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bi.Jennista Mhagama akisisitiza jambo katika kikao cha uzinduzi wa Bodi mpya ya Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC). Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Dkt.John Jingu na kushoto ni katibu mtendaji wa NEEC,Bi.Beng’i Issa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bi.Jennista Mhagama akikabidhi nyenzo za kazi kwa Mwenyekiti wa bodi ya Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC), Dkt. John Jingu katika kikao cha uzinduzi wa bodi hiyo mpya ya Baraza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na W,alemavu Bi.Jenista Mhagama akikabidhi nyenzo za kazi mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC), Prof.Samuel Wangwe katika kikao cha uzinduzi wa Bodi mpya ya Baraza hilo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi.Beng’i Issa akizungumza jambo katika kikao cha uzinduzi wa Bodi mpya ya Baraza hilo. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bi.Jennista Mhagama na wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NEEC, Dkt. John Jingu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...