Na Zainab Nyamka, 
Globu ya Jamii.

Baada ya ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Jang'ombe Boys zilizofungwa na mrundi Laudit Mavugo, timu ya Simba sasa itaumana na watani zao wa jadi Yanga katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la Mapinduzi unaotarajiwa kuwa Jumanne.
Ni katika kipindi cha kwanza dakika ya 11, Mavugo anawainua mashabiki wa Simba baada ya kuipatia goli la kwanza na la kuongoza.
Mpaka inafika mapumziko Simba walienda kifua mbele kwa goli 1-0, na katika kipindi cha pili Simba waliingia kwa kasi na katika dk  54 ni  mavugo  Tena  anaiandikia  simba  bao  la  pili  baada  ya kufanya  juhudi  binafsi  Kwa  kuwatoka  mabeki  wa Jangombe  boys  na  kuachia  shuti  lililomshinda  kipa.                           
 Dk ya 70 Jang'ombe walikosa bao la wazi baada ya shuti la Hafidh Bariki Juma kupanguliwa na kipa wa Simba ikamkuta Khamis Mussa Makame ambaye shuti lake lilitoka nje.  
Mpaka kufikia dakia 90 Simba wanatoka na ushindi wa goli 2-0 wakishika nafasi ya kwanza kwenye kundi A wakiwa na alama 10 na watakutana na Yanga kwenye mchezo wa nusu fainali.                      
 Jopo  la makocha  wa  timu  zote  mbili  limemchagua  laudit  mavugo  kuwa  man  of the mech  katika  mchezo  wa  leo.
 Kikosi cha Jang'ombe Boys kilichopambana jana na Simba katika mchezo wa hatua ya makundi uliomalizika kwa nSimba kupata ushindi wa goli 2-0.
Kikosi cha Simba Boys kilichopambana jana  na Jang'ombe Boys katika mchezo wa hatua ya makundi uliomalizika kwa Simba kupata ushindi wa goli 2-0.
 Shiza Kichuya akipambana na beki wa Jang'ombe Boys katika mchezo  wa hatua ya makundi uliomalizika kwa Simba kupata ushindi wa goli 2-0.
Jamali Mnyate akiwatoka mabeki wa Jang'ombe Boys wakati wa  mchezo  wa hatua ya makundi uliomalizika kwa Simba kupata ushindi wa goli 2-0.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...