WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Melinne saccos kuhakikisha wanakuwa wawazi na kutoa taarifa za hesabu za umoja huo kila wakati ili wanachama waweze kuwa na takwimu sahihi. 
Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Januari 11, 2017) wakati akizindua saccos hiyo yenye mtaji wa zaidi ya sh. bilioni moja kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinguzi Matukufu ya Zanzibar. 
Waziri Mkuu alisema viongozi hao wanatakiwa kuwa wawazi kwa wanachama wenzao jambo ambalo litawajengea uaminifu hivyo kuwezesha umoja huo kudumu na kufikia malengo yaliyokusudiwa. 
Alisema vyama vingi vya ushirika nchini vimekufa kutokana na viongozi wake kutokuwa waaminifu hivyo Serikali hatokubali kuona suala hilo linatokea katika umoja huo kwani litakwamisha maendeleo. 
Aidha, Waziri Mkuu aliwapongeza wananchi hao kwa kuanzisha saccos hiyo kwani wameweza kutimiza ndoto ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ya kuondokana na umasikini, dhuluma na unyonge.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,  Mama Asha Seif Idd kabla ya kufungua ukumbi wa SACCOS ya Melinne  mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shughuli za sherehe ya Mapinduzi ya Zanzibar 
 Waziri  Kassim Majaliwa , viongozi mbalimbali wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakimsikiliza  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd wakati  alipozungumza  baada ya Waziri Mkuu kufungua SACCOS ya Melinne mjini Zanzibar
 Baadhi ya wananchama wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua ukumbi wa SACCOS hiyo 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua SACCOS ya Melinne mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya shamrashamra  za sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar januari 11, 2017.   Kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd
 Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanachama wa SACCOS ya Melinne ya Zanzibar baada ya kufungua ukumbi wao Januari 11, 2017. Kulia kwake ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd. Habari kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...