Waziri
Mkuu, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa, MB. anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
kwenye harambee iliyoitishwa na Shirika lisilo la kiserikali la Land
O’Lakes ikilenga kukusanya fedha kwa ajili ya uwezeshaji wa wanawake
katika kilimo hasa kilimo biashara nchini kupitia taasisi iliyojikita
kwenye kuendeleza wanawake katika kilimo Tanzania (CAWAT).
Akizungumza
na waandiishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Mradi
wa Ubunifu Katika Maswala ya Kijinsia na Kuimarisha Uhakika wa Chakula
Katika Ngazi ya Kaya, unaoendeshwa na Land O Lakes, na kufadhiliwa na
Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Watu wa Merekani (USAID), Dk Rose
Kingamkono, alisema katika harambee hiyo Waziri Mkuu Majaliwa,ataungana
na wageni waalikwa wengine zaidi ya 200 na kwamba zaidi ya sh milioni
150 zinatarajiwa kukusanywa.
Alisema lengo la harambee hiyo inayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam Februari 17 mwaka huu ikiwa na kauli mbiu “WEZESHA KILIMO BIASHARA ILI KUKUZA AJIRA, JAMII NA VIWANDA ENDELEVU” ni
kukusanya kiasi hicho cha pesa kitakachosaidia kuijengea uwezo wa
kiutendaji taasisi hiyo mpya ya CAWAT iliyoanzishwa mahususi kusimamia
programu endelevu katika kumnyanyua mwanamke kupitia kilimo chenye tija
na ufanisi.
“Mwanamke
akijengewa uwezo wa kufanya shughuli za uzalishaji mali kwa ufanisi
atakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha ustawi wa familia na jamii
kwa ujumla, huku pia akiondoa kabisa tatizo la upungufu wa chakula na
lishe duni katika kaya zetu na hayo ndio malengo ya kuanzishwa kwa CAWAT
tunayoipigania sasa.
“Tafiti
zimeonyesha kwamba uchumi ulioshikiliwa mikononi mwa mwanamke huelekeza
matumizi yake kwa ajili ya ustawi wa familia zaidi kuliko ilivyo kwa
uchumi ulioshikiwa mikononi mwa mwanaume’’ alisema.
Alisema
taasisi hiyo ya CAWAT kwa sasa ipo kwenye mchakato wa awali wa kuanza
kujitegemea yenyewe kiuendashaji bila kutegemea msaada iliyokuwa
ikiupata kutoka kwenye mradi unaohusu ‘Ubunifu
katika masuala ya kijinsia na kuimarisha uhakikaka wa chakula katika
ngazi ya kaya (Innovations in Gender Equality (IGE), to Promote
Household Food Security unaotarajiwa kuisha Machi mwaka huu.
“Kuelekea
katika kujiendesha yenyewe bila kutegemea msaada inayoupata kutoka
mradi wa IGE, taasisi hii ya CAWAT bado ina safari ndefu inayohitaji
msaada kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ili iweze kutimiza
wajibu wake wa kuwasaidia wakina mama walio kwenye sekta hii muhimu ya
uzalishaji. Tunawaomba sana watanzania mmoja mmoja, taasisi, mashirika,
balozi mbalimbali waguswe katika kusaidia hili.’’ Alisema.
Mkurugenzi wa Mradi wa Ubunifu Katika Maswala ya Kijinsia na Kuimarisha Uhakika wa Chakula Katika Ngazi ya Kaya, unaoendeshwa na taaisisi ya Land O Lakes, na kufadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Watu wa Merekani (USAID), Dk Rose Kingamkono (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na harambee iliyoitishwa na taasisi hiyo ikilenga kukusanya fedha kwa ajili ya uwezeshaji wa wanawake katika kilimo biashara kupitia taasisi iliyojikita kwenye kuendeleza wanawake katika kilimo Tanzania (CAWAT). Wengine ni maofisa wa taasisi hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...