Na Shamimu Nyaki-WHUSM

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amewataka wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kufanya kazi kwa ari ili kuhakikisha linakuwa mfano Barani Afrika katika kuhabarisha umma.

Waziri Nape ameyasema hayo leo alipofanya ziara katika Shirika hilo ili kuona utendaji kazi pamoja na kuona changamoto mbalimbali zinazolikabili Shirika hilo.

“Fanyeni kazi kwa bidii na uadilifu kwa kutoa taarifa za ukweli na zenye uhakika kwa watazamaji puuzeni propaganda zinazoenezwa mtaani kuwa Shirika hili limepoteza Watazamaji na wasikilizaji kwa manufaa ya Taifa letu”.Alisema Waziri Nape.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Dkt.Ayoub Ryoba ameeleza kuwa Shirika linaendelea kuongeza wasikilizaji na watazamaji ambapo kuanzia mwaka 2012 hadi 2016 limeongeza mitambo kutoka kumi na mbili hadi hadi kumi na tisa iliyofungwa Mtwara,Rombo,Mbambabei na Tarime.

Aidha, Dkt Ryoba ameongeza kuwa Shirika hilo bado linaendelea kuwa katika historia ya Kuwa Shirika lililohabarisha umma juu ya Jitihada za Serikali ya Tanzania katika Ukombozi wa Bara la Afrika pamoja na kuendelea kukuza lugha ya Kiswahili kupitia kipindi cha malenga wapya.

“Shirika letu linaendelea kutoa habari, elimu na burudani zinazozingatia muktadha wa Utamaduni wa Nchi yetu ambapo kwa kipindi cha mwaka jana tumekuwa tukirusha matukio mubashara kupitia mitandao ambayo yana wafuatiliaji zaidi ya million tano.” Alisema Dkt.Ryoba.

Shirika hilo linaendelea kuwafikia watazamaji na wasikilizaji wengi zaidi ndani na nje ya nchi kwa kuendelea kuweka mikakati ya kuongeza vituo vingi zaidi.
 Makamu Mwenyekiti Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Bw. William Kalaghe Akimueleza jambo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye alipofanya ziara na kuongea na watumishi wa Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) Dkt. Ayoub Rhioba akimueleza jambo Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye wakati alipokutana na uongozi wa Shirika hilo wakati wa ziara na kuongea na watumishi wa Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye akiongea na uongozi wa Shirika la Utangazaji Taifa (TBC) alipofanya ziara ya  kuongea na watumishi wa Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...