Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye akiangalia mfumo wa zamani wa kuhifadhia magazeti alipotembelea Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara hiyo Bibi. Zawadi Msalla na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi, Katibu wa Waziri Bw. Octavian na Afisa Habari Mkuu John Lukuwi.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi akimuonyesha habari iliyoandikwa katika gazeti la Mzalendo la miaka ya nyuma Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) alipotemmbelea Ofisi za Idara hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari Mkuu wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. John Lukuwi akimuelezea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye ( aliyekaa) namna Kamera ya kupigia picha za majengo marefu inavyofanya kazi wakati wa ziara yake katika Ofisi za Idara hiyo leo jijini Dar es Salaam. Waliosimama wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo (Sehemu ya Habari) Bw. Artemony Tiganya.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Mozes Nnauye akiangalia saver kwa ajili ya kuhifadhi Picha za matukio mbalimbali alipotembelea Ofisi za Idara ya Habari (MAELEZO) leo jijini Dar es Salaam. kulia ni Afisa Habari Mkuu wa Idara hiyo Bw. John Lukuwi.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...