Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akikagua mfumo wa kielektroniki wa ukadiriaji na ulipaji kodi ya ardhi Wilayani Kilolo mkoani Iringa mara baada ya kuwasili wilayani humo mapema wiki hii kufuatilia utendaji wa sekta ya ardhi. Dkt. Mabula pia alikagua kumbukumbu za majalada za ulipaji kodi.Anayetoa maelezo ya ufanyaji kazi wa mfumo huo ni Afisa Ardhi wa Halmashairi ya Wilaya hiyo Bw. Elinaza Kiswaga.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula akisalimiana na wajumbe wa Baraza la Kata ya Mtitu Wilayani Kilolo mkoani Iringa mara baada ya kuwasili wilayani humo kufuatilia utendaji wa sekta ya ardhi. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Asia Juma Abdallah.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...