Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella akitoa hotuba yake katika halfla ya uzinduzi rasmi wa matawi mawil ya Bank of Africa Tanzania.

Akizungumza mkoani Mwanza, wakati akizindua matawi mawili kwa pamoja ya Bank of Africa Tanzania tawi la Nyanza lililopo jijini Mwanza na wakati huo huo tawi la Uluguru lililopo jijini Morogoro, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. John Mongella alisema ni wakati wa wanaMwanza kutumia huduma za kibenki na kwamba Mwanza ni ya pili kuchangia katika pato la taifa.

“Nimesikia kwamba mna matawi 27, huu ni wakati wa wanaMwanza kutumia huduma za kibenki. Naomba mfahamu kwamba Mwanza inachangia asilimia 7 ya pato la taifa. Bank of Africa Tanzania natambua kuwa mnasaidia juhudi za serikali kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi,”alisema Mh. Mongella.

Naibu Mkurugenzi mtendaji wa Bank of Africa Tanzania Wasia Mushi akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Mwanza zawadi ya Visa Prepaid Card (TOUCAN CARD) ambayo itamwezesha mkuu huyo wa mkoa kufanya online purchases pamoja na kupata huduma za kifedha kwenye ATM machine Zaidi ya Milioni tatu zilizopo sehemu mbalimbali duniani.

Awali akizungumza kabla ya ufunguzi wa matawi hayo kwa pamoja, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Wasia Mushi alisema : “Benki ya Afrika ipo katika nchi 18 na kwamba makao yake makuu yapo Dakar, Senegal. Hapa nchini ina makao yake makuu jijini Dar es Salaam na jumla ya matawi 27.”
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe John Mongella akizindua rasmi tawi la Nyanza-Mwanza na lile la Uluguru-Morogoro.

Mushi alisema katika kipindi cha miaka 10 benki hiyo imekuwa benki muhimu, imara endelevu kwa kutoa huduma zake za kibenki kwa watu mbalimbali wakiwamo wateja wakubwa, wadogo na wa kati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...