Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Baraza la Sanaa nchini (BASATA) limeziomba taasisi za Serikali na mashirika mbalimbali,kununua kazi za Sanaa za uchoraji za wasanii Watanzania na kuacha kununua michoro kutoka nje ambayo haina ubora.

Hayo yamesemwa na Afisa habari wa Basata, Agnes Kimwaga alipotembelea maonyesho ya wazi ya uchoraji wa michoro mbalimbali yaliyoandaliwa na kundi la 14 + la hapa nchini.

“Sanaa za uchoraji na uchongaji za hapa nchini zinatengenezwa katika ubora wa hali ya juu, ndio maana michoro mingi inayopelekwa nje kutoka hapa inapata sifa kubwa hivyo ni wakati wa tasisi zetu za umma na ofisi za serikali kuanza kupambwa na michoro hii” amesema Agnes.

Kwa upande wake kiongozi wa kikundi cha 14 +, Lutengano Mwakisopile amewataka watanzania kuendelea kuwaonga mkono katika harakati zao hili waweze kujivunia sanaa hiyo kama ilivyo kwa nchi jirani.
Kundi la wasanii wa uchoraji la 14+ ikiwa katika maonyesho ya uchoraji picha katika maeneo ya wazi.
Msemaji wa kundi la 14 +, Aman Abeid akitoa maelezo kwa afisa habari wa Barza la Sanaa nchini (BASATA) Agnes Kimwaga wakati wa maonyesho hayo
Mchoraji Nguli wa sanaa za uchoraji, Raza Muhamed akichora wakati wa maonyesho hayo ya uchoraji wa moja kwa moja katika eneo la wazi
Mchoraji Lutengano Mwakisopile akionyesha ufundi wake wa kuchora katika eneo la busatani ya kaburi moja Posta jijini Dar es Salaam
Mchoraji Chilonga Haji akionyesha umahiri wake wa kuchora katika maonyesho hayo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Basata ni muhimu sana ikawa na mipango mikaati yakufanya hilo kuwezekanika na liisiishie kwenye kupiga maneno tu!!Basata inaitaji kuwawekea mazingira mazuri wasanii ili waweze kuboresha kazi zao na kuwa katika kiwango cha kuzifanya kushindana ubora na kzi nyingine za nje ziizopo hapa nchini,basata inatakiwa ije na sera itakayohakikisha ulinzi wa kazi za wasanii wa ndani na kuzifanya azi za sanaa za nje kuonekana kuwa ghali ukilinganisha na za hapa ndani!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...