Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula amezindua uwekezaji mkubwa wa hoteli ya kisasa ambayo ndiyo kubwa kuliko zote Mkoani humo, Mazubu Grand Hotel iliyopo Mji mdogo wa Mirerani.
Akizungumza wakati akizindua hoteli hiyo, mhandisi Chaula amewataka wafanyabiashara na wachimbaji wa madini ya Tanzanite kuwekeza kwenye mji mdogo wa Mirerani kuliko kuchuma madini hayo na kwenda kuwekeza sehemu nyingine.
“Tunakupongeza mno ndugu yetu Elias Kipunile Maduhu kwa kufanikisha mradi huu kwani umetupa heshima kubwa watu wa wilaya hii ya Simanjiro kwani kwenye mkoa wote wa Manyara, hakuna uwekezaji mkubwa wa hoteli kama hii,” alisema mhandisi Chaula.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mazubu Grand Hotel Elias Kipunile Maduhu, alisema uzalendo wa kuishi Mirerani ndiyo umesababisha yeye awekewe kwenye eneo hilo kwani mahali unapoishi inakubidi upathamanimi kama nyumbani kwako.
Amesema Mazubu Grand Hotel imeshatoa ajira kwa watu 26 na lengo lao ni kuwapatia ajira watu 40 hadi 50 kwa siku za baadaye.
Zoezi la uzinduzi wa Mazubu Grand Hotel, likiwa limefanywa na Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhandisi Zephania Chaula kwa kukata utepe.
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara mhandisi Zephania Chaula na Mkurugenzi wa Mazubu Grand Hotel, Elias Kipunile Maduhu wakibadilishana mawazo baada ya kufanyika uzinduzi wa hoteli hiyo ya kisasa.
Jengo la Mazubu Grand Hotel ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ambao ni uwekezaji mkubwa kufanyika wa hoteli kwenye mkoa huo.
Mkugurenzi wa Mazubu Grand Hotel ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Elias Kipunile Maduhu, akizungumza mara baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo mhandisi Zephania Chaula kufanya uzinduzi wa hoteli hiyo ya kisasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...