Na  Bashir  Yakub.

Sheria  inayoshughulikia   habari  nzima  ya  madawa  ya  kulevya  inaitwa “The  Drug  Control  And  Enforcement  Act”.  Ni  sheria  namba  5  ya  mwaka  2015.  Ni  sheria  mpya  kabisa. Msanii  Wema  Sepetu  ni  kati  ya  Watu  walioko  mahakamani  tayari  kuamuliwa  kwa  mujibu  wa  sheria  hii.

1.AINA  YA  DAWA  ZA  KULEVYA.
Sheria  hii  inataja  aina  nyingi  mno  ya  vitu  ambavyo  imeviita  dawa  za  kulevya. Vipo  jamii  ya  kimiminika,  jamii  ya  unga,  jamii  ya  miti,  majani, mbegu  n.k.
Kifungu  cha  2   cha  sheria  hiyo  kinachosomwa  sambamba  na Schedule  ya 1  ya  sheria  hiyohiyo  kimeorodhesha  zaidi   ya  sampuli  100  ya  vitu  ambavyo  vinahesabika  kuwa   ni  dawa  za  kulevya hapa  Tanzania. Humo  imo  pia  bangi,  mirungi, cocaine, heroine na  aina  nyingine  nyingi.  Katika  hizi  Msanii  Wema  anatuhumiwa  kukutwa  na  misokoto  ya  bangi.

2.   JE  ILIKUWA  SAWA  WEMA  KUPEWA  DHAMANA  ?.
Ndio  ilikuwa  sawa.  Wako  watu  wanasema  kuna  mtu  amemkingia  kifua  akapata  dhamana. Hili si  kweli .  Dhamana  katika   kesi  za  madawa  ya  kulevya  hunyimwa  kutokana  na  kiwango  ulichokutwa au  unachotuhumiwa  nacho.   Kifungu  cha  29  cha  Sheria  hiyo  ya  kupambana  na  dawa  za  kulevya  kimeeleza  hilo  kama  ifuatavyo;.

( a ) Kama  ni  cocaine, heroine, mandrax, morphine, cannabis  resin au  opium   kuanzia gramu  200  au  zaidi  hakuna  dhamana.  Ni  pote  polisi  na  mahakamani.
( b ) Kama  ni  dawa  aina  ya  majani  au  mimea  kama  bangi n.k  kuanzia  kilo  100  au  zaidi  hakuna  dhamana. Ni  pote  polisi na  mahakamani.
( c ) Kama  ni  dawa  zenye  mfumo  wa  kemikali  kuanzia  lita  30 au  zaidi au  kilo  100  ikiwa  zimewekwa  katika  mfumo  wa  unga au  vinginevyo  hakuna  dhamana.  Ni  pote  polisi na  mahakamani.
Wema  Sepetu  alikutwa  na kiwango  kidogo kwa  taarifa  zilizotolewa,  ni  kama  msokoto  mmoja  hivi.  Ukiangalia  hapa  juu  hakuna  popote  ambapo kiwango  hicho  kimetajwa  kuwa hakidhaminiki.  Kwa  hiyo  kosa  lake  lilikuwa  la  kudhaminika  kabisa  kwa  mujibu  wa  kifungu  hiki.

3.   JE   WEMA  ANAKABILIWA  NA  ADHABU  ZIPI ?.

Kifungu  cha  17 ( 1 )  cha  Sheria  ya  Kuzuia  na  Kupambana  na  dawa  za  kulevya   kinaeleza  adhabu  ya  miaka  mitatu  jela, au  faini  isiyopungua  laki  tano   au  vyote  viwili.
Kwahiyo  panapo  kupatikana  na  hatia   atatakiwa  kwenda  jela  miaka  mitatu,  au  asiende  jela  iamuliwe  alipe  faini  inayoanzia  laki  tano  za  Tanzania,  au   aende  jela  miaka  mitatu  na  hapohapo  alipe na  faini  inayoanzia  shilingi  laki  tano  kwenda  mbele.

KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...