Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah (kulia) ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Liverpool akitoa uchambuzi wa timu hiyo kwenye barabara ya kuelekea Anfield wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba akizungumzia tukio adhimu la Benki ya Standard Chartered, Tanzania Limited kutimiza miaka 100 tangu ilipofungua milango yake nchini Tanzania kabla ya kumkaribisha Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Sanjay Rughani kutoa risala katika sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati wa sherehe za uzinduzi wa awamu ya pili ya mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017, barabara ya kuelekea Anfield uliofanyika katika viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa idara ya Fedha wa Benki ya Standard Chartered, Abdulrahman Said (wa pili kushoto) akizungumzia katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu ujio wa mchezaji aliyewika wa timu ya Liverpool, John Barnes ambapo wateja wa Benki hiyo watapata fursa ya kukutana na mchezaji huyo.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani (wa tano kulia) akimkabidhi zawadi Mchambuzi mkongwe wa kandanda nchini, Dr. Leaky Abdallah (wa tatu kushoto) ambaye pia ni mshabiki mkubwa wa Liverpool katika sherehe za uzinduzi huo. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mahusiano wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...