NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
KAIMU
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt.Tito
E. Mwinuka, (pichani kushoto), amefanya ziara ya kutembelea vituo vitatu vya kupoza na kusambaza
umeme wa msongo wa Kilovoti 132, (132Kv), vya Mbagala, Kurasini Wilayani Temeke
na Kariakoo Wilayani Ilala jijini Dar es Salaam leo Februari 4, 2016 na
kuwaomba wateja wa Shirika hilo kuwa wavumilivu wakati juhudi za kukamilisha
mradi wa uboreshaji umeme ukiwa unakaribia kukamilika.
Dkt.
Mwinuka alisema, ongezeko la watu na
shughuli za kiuchumi katika maeneo ya Mbagala, Kigamboni na Wilaya ya Mkuranga
Mkoani Pwani, kumepelekea upatikanaji wa umeme kwenye maeneo hayo kuwa na
matatizo kidogo kwani vituo vinavyosambaza umeme kwenye maeneo hayo vilikuwa na
ukubwa wa kupoza umeme wa Kilovoti 33 tu, na ndio maana TANESCO kupitia Mradi
wa uboreshaji umeme jijini Dar es Salaam unakaribia kukamilisha ujenzi wa vituo
vilivyotajwa hapo juu ili view na uwezo mkubwa wa Kilovoti 132 na hivyo kuondoa
kabisa tatizo hilo.
“Barabra
zinapozidiwa na magari ni rahisi sana kubaini kutokana na ongezeko la magari
yanayotumia barabara hizo, lakini ongezeko la watumiaji umeme na shughuli za
kiuchumi inakuwa vigumu kubaini kwa haraka, kwa hivyo niwaombe wateja wetu kuwa
wavumilivu kwani tatizo hilo litakuwa limepatiwa ufumbuzi katika kipindi kifupi
kijacho.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Dkt.
Mwinuka pia aibainisha, kuwa kazi ya kuongeza ukubwa wa vituo vya kupoza na
kusambaza umeme inaendelea kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi ambako nako vituo
vya sasa vya ukubwa wa Kilovoti 33, vinabadilishwa na kuwa na uwezo wa
Kilovolti 132.
Dkt.
Mwinuka amewapongeza wakandarasi kwa juhudi kubwa wanazofanya katika
kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa haraka ili kuwaondolea adha wateja wa
Shirika hilo wa upatikanaji wa umeme ulio bora na wa uhakika.
Dkt. Mwinuka (kulia), akipatiwa maelezo ya litaalamu na Mkuu wa miradi (anayeshughulikia usafirishaji) wa TANESCO, Mhandisi Frank Mashalo, alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Februari 4, 2017. Wakwanza kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji.
Mitambo ya kupoza na kusafirisha umeme kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam, kikiwa katika hatua za mwisho ukamilika
Dkt. Mwinuka, (wapili kulia), akimsikiliza mkandarasi kutoka kampuni ya FICHTNER, ambaye ndiyo Menenja mradi, Mathias Alby, wakati alipotembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Mbagala, Wilayani Temeke jijini Dar es Salaam.
Habari zaidi BOFYA HAPA
Habari zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...