Kamati ya Bunge ya Hesabu
za Serikali (PAC) imekutana nakufanya kikao na Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC) kupokea taarifa ya maendeleo ya miradi ya TPDC mjini Dodoma.
Wataalam wa TPDC katika
kikao hicho walipata fursa ya kuwasilisha mada za taarifa ya maendeleo ya miradi
ya Shirika hilo.
Aidha,
katika kikao hicho Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC Prof. Sufian Bukurura
na Mkuu wa Taasisi ya Utafiti (REPOA) Dk. Donald Mmari waliwasilisha mada
kuhusu utafiti walioufanya kuhusu Shirika la Mafuta la Taifa linavyoweza
kujiendesha kwenye mazingira ya sheria mpya nchini.
Akihitimisha
kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Mhe. Naghenjwa Kaboyoka alisema kuwa
Kamati yake imepokea taarifa ya maendeleo ya miradi ya TPDC na kwamba Kamati
itakaa nakuifanyia kazi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC) Mhe. Naghenjwa akifungua kikao kulichoikutanisha Kamati ya PAC
na TPDC mjini Dodoma
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC,
Prof. Sufian Bukurura akiwasilisha mada mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC) katika kikao kilicho ikutanisha Kamati hiyo na TPDC mjini
Dodoma.
Mkuu wa Taasisi ya Utafiti (REPOA) Dk.
Donald Mmari akiwasilisha Mada mbele ya Kamati ya PAC mjini Dodoma
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya
Hesabu za Serikali (PAC) wakimsikiliza mtoa mada kutoka TPDC katika kikao
hicho.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...