Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimjulia hali jana, Jackson Kimambo
ambaye amelazwa katika hospitali ya KCMC Moshi mkoani Kilimanjaro baada
ya kupata ajali wakati akiendesha gari kutoka kwenye Maadhimisho ya
miaka 40 ya CCM mkoani humo, Jumapili, Feb 5, 2017. Katika ajali hiyo
watu sita walikufa wakiwemo viongozi wanne wa CCM ambapo Kinana yupo
mkoani hapa, kuongoza mazishi ya vingozi hao. Wapili kushoto ni Mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro Sid Mecky Sadick
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaini kitabu ha wageni Ofisini
kwa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya KCMC ya Moshi, Kilimanjaro, Dk.
Gileard Masenga (kulia), baada ya kumjulia hali dereva huyo
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya KCMC ya Moshi, Kilimanjaro, Dk. Gileard
Masenga, akiwaaga Katibu Mkuu wa CCM Abdulraman Kinana na Mkuu wa mkoa
wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadick
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro
Said Mecky Sadick, baada ya zara hiyo ya kumjulia hali, dereva huo.
PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...