
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akitoa salam za rambirambi zake binafsi, CCM na za Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli wakati wa mazishi ya aliyekuwa Katibu wa Hamasa wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu mkoa wa Kilimanjarona Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, Edwin Mselle, wakati wa ibada na kuaga mwili.
Mazishi hayo yamefanyika leo Wilayani Kibosho, mkoani Kilimanjaro. Edwin ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa udaktari, mwaka wa nne katika Chuo Kikuu Kishiriki cha KCMC, ni miongoni mwa viongozi wanne wa CCM waliofariki kwa ajali ya gari, wakati waitoka kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya CCM, Februari 5, 2017 ambapo Kinana ameongoza kwenye mazishi yao wote.

Taratibu zikifanywa na Padre kabla ya kuingiza jeneza kaburini

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiweka udongo kaburini

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick akimwaga udongo kaburini wakati wa maziko

Kinana akikabidhi rambirambi kutoka CCM na Jumuia zake kwa Baba wa Marehemu Edwin, Christopher Mselle wakati wa mazishi hayo

Kinana akimpa pole Padre Dackshen Hangai wakati wa mazsihi hayo.

Vijana wa UVCCM wakiwa wamebeba jeneza kwenda eneola maziko, wakati wa mazishi hayo .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...