SERIKALI imewataka Maafisa Habari na Maafisa Tehama katika sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya nchini kuweka taarifa sahihi zenye kuzingatia muda na wakati ili kuongeza ufanisi wa kutangaza shughuli za Serikali kwa umma.
Hayo yamesemwa leo Jijini Mwanza na Katibu Tawala wa Mkoa huo, C.P Clodwig Mtweve, katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala Msaidizi, Johnsen Bukwali wakati wa mafunzo elekezi ya uwekaji wa taarifa katika tovuti yaliyoandaliwa na Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Umma (PS3) kwa Maafisa Habari na Tehama wa Halmashauri na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera na Simiyu.
Kwa Mujibu wa C.P Mtweve alisema uwekaji taarifa katika tovuti hizo zitasaidia kuimarisha shughuli za utawala na kuifanya Serikali kufahamika zaidi kwa wadau wake na hivyo kupunguza malalamiko ya mara kwa mara yanayotolewa na wananchi kuhusu huduma zake kwa umma.
“Ninyi ndio mmekuwa wachakataji wa taarifa za Serikali na kuhakikisha zinaufikia umma wa Watanzania zikiwa katika hali ya ubora kwa kutumia njia mbali mbali za mawasiliano kama vile mbao za matangazo na hata kwa njia ya mitandao” alisema C.P Mtweve.
Kwa mujibu wa C.P Mtweve alisema kuwa lengo la Serikali ni kuongeza uwazi na wigo wa upatikanaji wa taarifa sahihi na zenye uhakika katika tovuti zake ili kuiepusha Serikali na habari za kuzusha na zisizo na maslahi kwa taifa.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Rebecca Kwandu akizungumza na wajumbe wa kikao cha mafunzo ya Maafisa Habari na TEHAMA kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera na Simiyu wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Jijini Mwanza. Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa huo, Johnsen Bukwali.
Mkuu wa Kitengo cha Mifumo ya Mawasiliano ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta ya Umma, Desderi Wengaa akizungumza na wajumbe wa kikao cha mafunzo ya Maafisa Habari na TEHAMA kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Kagera na Simiyu wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Jijini Mwanza. Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa huo, Johnsen Bukwali
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Mwanza, Johnsen Bukwali katikati (walipokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina ya mafunzo elekezi kwa Maafisa Habari na TEHAMA kutoka katika Hallmashauri na Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Kagera na Mara mara baada ya kufungua mafunzo hay oleo Jijini Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...