Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro wakati  aliposimama  akitoka  Orkesimet kwenda  Mererani Februari 16, 2017.
 Mwananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro  akiwasilisha kero yake kwa njia ya bango akidai mawasiliano ya simu za mkononi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  aliposimama na kuwasalimia wananchi wa kijiji hicho waliokusanyika  barabarani. Alikuwa akitoka  Orkesimet kwenda  Mererani Februari 16, 2017.
  Wananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati aliposimama na kuwasalimia akitoka  Orkesimet kwenda  Mererani Februari 16, 2017.
 Baadhi ya wananchi  Mererani mkoani Manyara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia  katika mkutano wa hadhara  kwenye uwanja wa mikutano wa Mererani ,  Februari 16, 2017.
 aziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wingi wa mabango  katika mikutano ya hadhara  ya viongozi wakuu ni ishara ya wazi kuwa  watendaji wa  Halmashauri  hawawatembelei  wananchi na kutatua kero zao. Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mikutano wa  Mererani mkoani Manyara Februari 16, 2017, Mheshimiwa Majaliwa alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro na watendaji wake kukusanya mabango  yaliyokuwa yakionyeshwa na wananchi kwani mengi ya matatizo yanapaswa kumalizwa na viongozi hao  na aliwaagiza  kurejea Mererani siku inayofuata ili waitishe mkutano na  kujibu bango moja baada ya jingine.
Pichani,  watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro wakikusanya mabango hayo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Ndugu Ali Juma baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara  kwenye uwanja mikutano  wa Mererani mkoani Manyara Februari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...