Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewataka wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuibua mbinu mpya zitakazosaidia kukabiliana na changamoto zinazolikabili bonde la Ziwa Victoria ikiwemo uchafu wa ziwa hilo unaotokana na shughuli za kibinadamu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo 15-Feb-2017 wakati anafungua mkutano wa siku Mbili unaojuisha wadau wa mazingira, wasayansi na watafiti wa bonde la Ziwa Victoria Jijini Mwanza.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema anaimani kubwa kuwa mkutano huo utakuwa ni chachu katika kuibua mbinu mpya na bora za kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaoendelea katika Bonde la Ziwa Victoria.

Amehimiza kuwa kutokana na muhimu wa bonde hilo ni vyema wadau wote katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kujumuika pamoja katika kulinda na kuendeleza uhifadhi wa bonde hilo kwa ajili ya manufaa ya wananchi wa jumuiya hiyo.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema bonde la Ziwa Victoria bado linakabiliwa na changamoto nyingi hasa kuibuka tena kwa magugumaji ambayo yameathiri shughuli za uvuvi, usafiri na kuchafua maji katika Ziwa hilo hivyo ni muhimu kwa makundi yote wakiwemo wanasayansi na watafiti kuweka mikakati mipya ya kukabiliana na changamoto hizo ambazo ni tishio kwa uhai wa Ziwa Victoria.

“Kufanya Maamuzi kwa kuzingatia ushauri wa kisayansi ni jambo zuri na la msingi katika kutunga sera ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kulinda na kuhifadhi Bonde la Ziwa Victoria kwa ajili ya manufaa ya wananchi wote”amesisitiza Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza anaimani kubwa kuwa majadiliano yatakayofanyika katika mkutano huo yatakuja na mbinu mpya ambazo zitatumika katika kuhifadhi na kuendelea Bonde la Ziwa Victoria.

Katika Mkutano huo wa siku Mbili unaofanyika Jijini Mwanza jumla ya mada 44 zitawasilishwa na kujadiliwa kwa kina na wadau wa mazingira, wanasayansi na watafiti.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan pia alitembelea mabanda mbalimbali ya maonyesho katika viwanja vya hoteli ya Malaika uliyopo Jijini Mwanza.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Mwanza
15-Feb-2017

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
. Sehemu ya watu waliohudhuria wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akitafakari jambo kabla ya kuanza kwa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Augustine Mahiza akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwa na (kushoto) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Augustine Mahiga pamoja na (kulia),Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Injinia wakiwa wamesoma kwa pamoja kabla ya kuanza kwa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau wa Mazingira Wanasayansi na Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria uliofanyika kwenye Hoteli ya Malaika jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...