Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameunga mkono jitihada za kupambana na dawa za kulevya nchini kama hatua ya kuliokoa na taifa janga hilo ambalo limesababisha madhara makubwa katika jamii.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.Makamu wa Rais amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya yatakuwa ni endelevu lengo likiwa kukomesha kabisa uuzaji,usambazaji na utumiaji wa dawa hizo kama hatua ya kuokoa kizazi cha sasa na kijacho nchini.

Amesema kamwe serikali ya wamu ya Tano hatarudi nyuma katika vita dhidi ya dawa za kulenya na ameomba wananchi waendelee kutoa taarifa za siri kwa vyombo vya dola zitakazosaidia kuwabaini watu wanajihusisha na biashara hiyo ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kuhusu tatizo la uvuvi haramu, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi wa mikoa ya kanda ya Ziwa wakiwemo viongozi wa Mwanza na mikoa mingine nchini kuanzisha mara moja oparesheni kali ya kupambana na wavuvi haramu katika Ziwa Victoria ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa samaki katika Ziwa hilo.

“Viwanda vya samaki kwa sasa havipati samaki wa kutosha hali ambayo imezorotesha shughuli za kuchakata samaki hivyo nawaagiza viongozi wote kupambana ipasavyo na wavuvi haramu na kamwe wasionewe huruma” amesisitiza Makamu wa Rais.

Makamu Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini ni muhimu yakaenda pamoja na oparesheni ya kukomesha uvuvi haramu katika Ziwa Victoria na maeneo mengine nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia Watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe. Angelina Mabula (kulia) wakati wa mkutano wa Makamu wa Rais na Watendaji  wa Halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akihutubia mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa watendaji na Halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Picha ya pamoja.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...