Timu ya Taifa ya Misri imetinga hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kufanikiwa kuitoa timu ya Burkina Faso kwa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia kumalizika kwa dakika 120 za mchezo huo kumalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana goli 1-1.
Mchezo huo uliomalizika hivi punde, ulikuwa ni wenye mvuto wa aina yake huku timu zote zikioneshana uwezo wa kushambuliana kwa zamu. Misri ndio walioanza kuliona lango la wapinzani wao mnamo dakika ya 66 kupitia kwa Mshambuliaji wake, Mohamed Salah na dakika saba baadae Burkina Faso walisawazisha goli kupitia kwa Aristide Bance.
Misri sasa itamsubiria mshindi wa mechi ya nusu fainali ya pili itakayopigwa hapo kesho kwa kuwakutanisha miamba wawili ambao ni Cameroon na Ghana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...