Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo(kushoto)akipokea kutoka kwa Mhandisi Shin Pil Soo sehemu ya msaada mabati 300 na mifuko ya Sementi 500 iliyotolewa na Kampuni ya ujenzi ya Hanil Jiangsu Joint Venture Ltd inayojenga barabara ya Sakina hadi Tengeru yenye urefu wa kilometa 14.1 ,kulia ni Meneja wa Tanrods mkoa wa Arusha,Mhandisi John Kalupale,msaada huo umetolewa kwa Mkuu wa mkoa ili umwezeshe kusaidia shughuli za maendeleo zilizoanzishwa na wananchi na alikabidhi ili utumike kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Makuyuni wilayani Monduli. 
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo akishirikiana na askari wa JKT kambi ya Makuyuni na wananchi wa Kata ya makuyuni katika ujenzi wa Kituo cha Afya katika ziara yake wilayani Monduli. 
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo(kushoto) akiwa na viongozi wa wilaya ya Monduli ndani ya moja vya vyumba viwili madarasa vilivyozinduliwa baada ya ujenzi wake kukamilika katika Shule ya Sekondari Rifit Valley. 
Wananchi wakichangia nguvu zao katika ujenzi wa jengo la Upasuaji kwenye Kituo cha Afya Mto wa Mbu 
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo akishiriki kazi za mikono pamoja na wananchi katika ujenzi wa jengo la upsuaji katika Kituo cha Afya Mto wa Mbu aliahidi kutoa mifuko 100 ya Sementi na Mabati 100. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...