Na Mathias Canal, Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela ameongoza mamia ya wananchi waliojitokeza kijijini Misasi, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kwa ajili ya kusindikiza safari ya mwisho ya kurejea mavumbini kwa utimilifu wa vitabu vitakatifu vya Dini Mzee Anton Raphael Kayombo.
Rc Mongela akiaga mwili wa marehemu Mzee Kayombo
Akizungumza kwa niaba ya wakurugenzi wote nchini Mkurugenzi wa Jiji la
Mwanza Kiyomondi Kibamba alisema kuwa msiba huo umekuwa pigo kwa familia ya
Kayombo na ukoo mzima lakini pia ni pigo kwa wananchi wote wa Kijiji cha Misasi
na Mkoa wa Mwanza kwa ujumla kwa kumpoteza mlezi na mshauri mzuri.
MD Kayombo amewashukuru madaktari wa hospitali zote waliojaribu kuokoa uhai
wa Mzee Raphael Kayombo hata hivyo ameeleza kuwa idadi kubwa ya watu
waliohudhuria Kwenye mazishi imeonyesha kwamba Marehemu Mzee Kayombo alikuwa na
mahusiano na kuishi vizuri na majiraji zake.
Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo ameacha watoto10, Wajukuu 60 na Vitukuu
30 huku kukiwa na idadi kubwa ya vilembwe.
Rc Makonda akiaga mwili wa marehemu Mzee Kayombo
Rc Mongela alisema kuwa kifo cha Mzee Kayombo kimeacha alama kubwa Duniani kwa ufanisi mkubwa alioufanya akiwa hai ambapo pia ni alama kubwa ya taswira ya fikra huru zitakazoishi kwa Yale aliowaasa wananchi katika maelekezo mbalimbali ikiwemo ushauri katika serikali.
Mongela aliyeambatana na mkewe katika mazishi hayo amewapongeza wananchi wote kwa kujitokeza mwenye mazishi hayo sambamba na kuwasihi kuendelea kutoa mshikamano kwa serikali katika majukumu mbalimbali ikiwemo kusimamia na kudumisha umoja waliouonyesha katika mazishi ya Mzee Kayombo.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alisema kuwa Mzee wake Hugo atakumbukwa kwa mambo mbalimbali aliyoyafanya wakati wa uhai wake pindi alipokuwa kazini ikiwa ni pamoja na kupanda miti katika shule zote alizofundisha, Ujenzi wa shule wakati huo, pia atakumbukwa kwa kuhamasisha ujenzi wa Zahanati ya Misasi.
Ameeleza kuwa Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kibofu cha mkojo ambao ulianza ghafla tarehe 29/1/2017 na kupelekwa katika hospital ya Misasi, Baadae hospitaliti ya Sekou Ture na mwishowe Hospitali ya Bugando ambapo alifanyiwa upasuaji ambapo hata hivyo hali yake iliendelea kudhoofika mpaka mauti ilipomkuta tarehe 4/2/2017 majira ya saa mbili usiku.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...