Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limeendeleea kuwashikilia Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusufu Manji na Askofu Josephat Gwajima kwa zaidi ya saa 24 mpaka sasa.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro amesema kuwa watu hao jana walifika hapo na kukutana na wapelezi .
“watu hawa wamehojiwa kuanzia jana mpaka saa za usiku kisha wakawekwa mahabusu hivyo mpaka sasa ninavyozungumza wapo mahabusu wakisubiri utaratibu mwingine” amesema kamanda Siro.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...