Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam,Paul Makonda amewataja watuhumiwa 65 wa Dawa za Kulevya. Katika majina hayo ametajwa Freeman Mbowe, Mchungaji Gwajima, Yusuf Manji na mbunge mstaafu Idd Azzan.
Akizungumza
na waandishi wa habari Ofisi kwake mapema leo jijini Dar,RC Makonda
ameingia katika awamu ya pili ya kutaja majina hayo na kuyaweka hadharani,huku akieleza kuwa watuhumiwa hao watatakiwa kufika kituo cha polisi kati
siku ya Ijumaa,saa tano asubuhi kwa mahojiano zaidi.
Katika
hatua nyingine RC Makonda amekiri kukamatwa kwa Mmiliki wa kituo cha
Radio ya EFM, ajulikanae kwa jina la Francis Ciza, almaarufu kwa jina la Dj
Majay."tulipokuwa tukifanya opereseheni ya kuwakamata Wahusika wote wa Dawa za kulevya juzi usiku nae akakamatwa kwa mahojiano zaidi;"alisema Makonda.
Makonda amejibu habari za kukamatwa kwa Dj Majay mara baada ya kuulizwa swali na mmoja wa waandishi wa habari, kufuatia tetesi nyingi zilizokuwa zikisambazwa kwenye
mitandao mbalimbali ya kijamii.
Soma zaidi majina ya watuhumiwa wa sakala hilo la Dawa za kulevya.
Soma zaidi majina ya watuhumiwa wa sakala hilo la Dawa za kulevya.





ukisoma vizuri kwenye list SIO FREEMAN MBOWE ni PHILEMONI MBOWE ambaye ni mtu tofauti....
ReplyDeletemtoa maoni Sakaya :usijaribu kupotosha ukweli sikiliza video ya majina yanayotajwa ni Mbowe gani aliyetajwa ! jibu ni mbunge wa Hai,sasa yupi?
ReplyDelete