
Habari ilizoifikia Globu ya Jamii jioni ya leo kutoka Mkoani Kilimanjaro,zinaeleza kuwa watu zaid ya watano wanadaiwa kupoteza Maisha,akiwemo mwandishi wa habari wa gazeti la Habarileo na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Hai,Anord Swai,katika ajali ya gari dogo.Ajali hiyo inaelezwa kuwa imetokea maeneo ya Mwika Mawanjeni maarufu kama Bar Mpya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Inaelezwa kuwa ndani ya gari hiyo walikuwemo watu sita wakiwemo viongozi wa CCM wakitoka kushiriki sherehe za miaka 40 ya CCM kimkoa yaliyofanyika katika ukumbi wa shule ya Msingi Shauri Tanga wilayani Rombo.Chanzo cha ajali inaelezwa kuwa ni fuso kufeli breki na kuligonga gari dogo.
“Waliofariki ni Mwenyekiti wa Uvccm wilayani Hai na Mwandishi wa habari Leo Arnold Swai, mjumbe wa NEC ya CCM na Katibu wa CWT mkoa wa Kilimanjaro Ally Mmbaga na wanafunzi makada wa CCM kutoka vyuo vikuu vya ushirika na KCM.
Majeruhi wa ajali hiyo ni Jackson Kimambo ambaye inaelezwa kuwa amekimbizwa Hospitali kwa matibabu,Watu hao walikuwa wakitoka kwenye maadhimisho ya kilele cha miaka 40 ya kuzaliwa CCM wilayani Rombo”
Pichani ni aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai na mwandishi wa habari wa gazeti la serikali la Habari leo,enzi za uhai wake,Arnold Swai ambaye pia ni mmojawapo kati ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.
Globu ya Jamii itazidi kuwaletea habari zaidi kutoka katika mamlaka husika,hususani Jeshi la Polisi.
Mungu azilaze Roho za Marehemu Mahali pema peponi-Amin,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...