Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeendesha semina maalum kwa
waajiri wake wa mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu endelevu
waliojipangia kukutana na waajiri wake ili kuendelea kuelezana
umuhimu wa hifadhi ya jamii kwa waajiriwa wao na pia kupata fursa ya
kuambiana changamoto kutoka pande zote ili kushirikiana kuzitatua na
kuboresha huduma kwa pande zote.
Akiwakaribisha waajiri hao katika semina hiyo, Meneja wa NSSF mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma aliwaambia waajiri hao kuwa huo ni urataribu endelevu waliojipangia wa kukutana nao na kuwataka watekeleze wajibu wao wa kuwaandikisha wanachama na kuleta michango kwa wakati ili kuwezesha Shirika kutoa mafao kwa wanachama wao kwa wakati na kwa usahihi na kuwakumbusha kuhusu sheria ya NSSF inayoruhusu kutoa adhabu kwa waajiri wanaposhindwa kuwasilisha michango kwa wakati.

Awali, Meneja Matekelezo wa Shirika hilo, James Oigo aliwaambia waajiri hao kuwa swala la hifadhi ya jamii ni muhimu kuliko ambavyo mtu anaweza kufikiri kwa kuwa kuna mfano wa wazee wengi ambao mnawajua wanaishi maisha duni kutokana na kutokuwa katika mfumo wa hifadhi ya jamii.
NSSF
imeendelea kuwa kinara katika mifuko ya hifadhi ya jamii katika wingi
na ubora wa mafao na sasa imeelekeza nguvu zake katika uwekezaji wa
viwanda kama fursa ya kuendelea kuboresha mafao ya wanachama wake,
kuongeza ajira na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.
Meneja
Matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), James Oigo
akitoa Mada wakati wa Semina semina maalum kwa waajiri wake wa mkoa wa
Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu endelevu waliojipangia wa kukutana
na waajiri hao, iliyofanyika katika Ukumbi wa Veta, Mjini Dodoma.
Meneja
wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) mkoa wa Dodoma, Rehema
Chuma akizungumza wakati wa Semina semina maalum kwa waajiri wake wa
mkoa wa Dodoma ikiwa
ni sehemu ya utaratibu endelevu waliojipangia wa kukutana na waajiri
hao, iliyofanyika katika Ukumbi wa Veta, Mjini Dodoma.
Kaimu
Meneja Kiongozi wa Uhusiano na Masoko wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF), Salum Kimaro akitoa maelezo kwa wanasemina hao,
iliyofanyika katika Ukumbi wa Veta, Mjini Dodoma.
Washiriki wa semina wakiajiandikisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...