Ikiwa Operesheni Lipa Kodi ya Pango la Ardhi inaendelea,
ambapo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
inaendelea kutoa notisi ya siku 14 kwa wadaiwa sugu wa Kodi ya
pango la Ardhi huku ikiendelea na kuhabarisha Umma kuhusu
umuhimu wa kuzingatia Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999,
katika vifungu Na. 49 na 51 ambavyo vinadhihirisha ruhusa ya
mmiliki kufutiwa umiliki wa ardhi kama mmiliki hatazingatia kulipa
Kodi ya Pango la Ardhi.
Kwa upande wake; Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendelea ya Makazi, Dkt Angeline Mabula (Mb), amekuwa
akifanya ziara ya kukagua mifumo ya ulipaji kodi ya pango la
Ardhi sehemu mbalimbali nchini.
Katika picha ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelea ya
Makazi, Dkt Angeline Mabula (Mb) akikagua mifumo ya ulipaji
kodi ya pango la Ardhi sambamba na kuhakiki kumbukumbu za
umiliki wa Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani
Mwanza. Alioambatana nao ni Maafisa Ardhi na Afisa TEHAMA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...