Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
JAJI Mkuu anatarajia kupokea orodha ya majina ya mahakimu na majaji ambao wanadaiwa kuvuruga kesi za watu wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.
Hayo ameyasema leo Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Rogers Sianga wakati wa mkutano wa viongozi mbalimbali wa kitaifa na waandishi wa habari ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa ajili kupambana na dawa za kulevya.
Sianga amesema kuwa kesi zimevurugwa na mahakimu na majaji. hivyo wale wote watakaobainika kuhusika watashitakiwa na hata wawe na mali ambazo wamezipata kwa biashara hiyo zitataifishwa.
Amesema kuwa watazunguka katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ili kuhakikisha mtandao huo unapatikana na kwenda hata Zanzibar na mbinu zote wanazijua katika kufanya biashara hiyo.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemkabidhi orodha ya majina 97 wanaojihusisha na dawa za kulevya na kuongeza kuwa moto umewashwa dhidi ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya.
Amesema kuwa kuna nyumba 200 zinajihusisha kufanya biashara ya madawa ya kulevya hapa jijini ambapo wote hao watafikiwa katika operesheni,ambayo mojawapo wanatarajia kuifanya usiku wa leo.
Nae Msanii wa muziki wa kizazi kipya Khalid Mohamed almaarufu kwa jina la kisanii TID , amesema kuwa sasa ni mnyama ambae yuko tayari kupambana na watu wanaouza pamoja na kutumia dawa za kulevya na amerudi kwa kufanya kazi na kuongeza kuwa kuimba hakuitaji dawa za kulevya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...