Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla hajapanda ndege na kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla hajapanda ndege na kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kabla ya kuondoka ma kurejea nchini kwake.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo za Mataifa mawili
zilipokuwa zikipigwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Terminal 1.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakifurahia
jambo wakati walipokwenda kumsindikiza Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni
katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...