Na:
Lilian Lundo – MAELEZO - Dodoma
Waziri
wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo amesema kuwa msimamo wake juu ya Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco)
kutopandisha gharama za umeme kwa wateja wake upo palepale.
Prof.
Muhongo ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu hoja
zilizowasilishwa na wabunge juu ya zuio
la upandishaji bei ya umeme kwa shirika hilo wakati wa uwasilishwaji wa taarifa
ya shughuli za Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini katika kipindi cha
mwaka 2016/2017.
“Haiwezekani
wakapandisha bei ya umeme wakati kuna watu ndani ya Shirika wanamiliki hadi
hoteli nne, wakijaza lita 20 za mafuta katika magari wanaandika lita 50 na kila
mwisho wa mwaka wanagawana milioni 50 kama ‘bonus’,” alifafanua Prof. Muhongo.
Ameendelea
kwa kusema kuwa Shirika hilo linadaiwa kiasi cha shilingi Bil. 820, katika deni
hilo kiasi cha shilingi Bil.320 bado hazijachambuliwa. Hivyo shirika hilo
haliwezi kujiamulia kupandisha gharama ya umeme wakati huo huo wakiwa bado hawajachambua
baadhi ya madeni yao.
Aidha
Prof. Muhongo amesema kuwa, Shirika hilo linahitaji kiasi cha Dola Bil. 12 kwa
ajili ya uwekezaji ili ifikapo mwaka 2020 kiasi cha Mg 5000 za umeme ziweze
kuzalishwa.
Hata
hivyo, Prof. Muhongo amesema amekwisha anza kufanya mazungumzo na Benki ya
Dunia ili kuona kama wataweza kufadhili kiasi hicho cha fedha ili kiweze kuwekezwa
katika Shirika hilo.
Aliendelea
kwa kusema kuwa Shirika hilo linahitaji mabadiliko ya hali ya juu ili kulifanya
kuwa la kisasa na kuendana na dhima ya nchi ya uchumi wa viwanda ambao kwa asilimia kubwa
unahitaji nishati hiyo ya umeme.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...