JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo  : “N G O M E”        Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo: DSM 22150463     Sanduku la Posta 9203,
Telex                   : 41051                       DAR ES SALAAM, 31 Januari, 2017.
Tele Fax              : 2153426
Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa na taarifa iliyotolewa na gazeti la Tanzania Daima toleo Nambari 4438 la tarehe 28 Januari 2017, Habari leo   la tarehe 29 Januari 2017 na baadhi ya vyombo vya habari vikihusisha mauaji ya kondakta wa daladala na Wanajeshi Mkoani Tanga.

Tunapenda  kuwataarifu wananchi kwamba kwa mujibu wa jeshi la polisi watuhumiwa wanaoshikiliwa na Jeshi hilo ni wanne (4),mmoja kati yao ni Mwanajeshi ambaye ni mzazi wa msichana anayetuhumiwa kusababisha tukio hilo. 

Hivyo Mwanajeshi huyo anashikiliwa kwa ajili ya kulisaidia Jeshi la Polisi katika uchunguzi kwa kuwa tukio hilo lilifanyika nyumbani kwake. Hakuna Wanajeshi waliohusika katika tukio hilo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari, kambi za Jeshi wanaishi Wanajeshi pamoja na familia zao hivyo kuhusisha moja kwa moja mauaji hayo na Wanajeshi  mkoani Tanga ni kuupotosha umma.

Wito unatolewa kwa vyombo vya habari kuripoti habari zenye ukweli.Habari zisizo za kweli zinapotosha umma na kujenga taswira potofu kwa wananchi dhidi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.  

Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ni aibu jeshi kutumia yahoo account kwenye official email. Siri za jeshi zinaweza kuvuja kirahi , nawaomba tafadhali badilisha haraka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...