JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA
YA NISHATI NA MADINI
TAARIFA
KWA UMMA
AWAMU
YA KWANZA YA WATUMISHI KUHAMIA MAKAO MAKUU YA NCHI - DODOMA TAREHE 10 FEBRUARI,
2017
Wizara ya Nishati na
Madini inapenda kuufahamisha umma kuwa, Awamu ya Kwanza ya Watumishi wa Wizara
kuhamia Makao- Makuu ya Nchi, Dodoma inaanza tarehe 10 Februari, 2017.
Miongoni mwa watakao
hamia katika awamu hiyo ni pamoja na Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara
ambao ni Waziri wa Nishati na Madini, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Naibu Makatibu Wakuu wa Nishati na
Madini.
Watumishi wengine ni
pamoja na Kamishna wa Madini Tanzania, Kamishna wa Nishati na Masuala ya
Petroli, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Maafisa. Jumla ya Watumishi
wanaohamia Dodoma Awamu ya Kwanza ni 47.
Aidha, kutokana na
uhamisho huo, anuani ya Wizara Dodoma
ni;
Katibu Mkuu,
Wizara ya Nishati na
Madini,
Barabara ya Kikuyu,
S.L.P 422,
DODOMA
Imetolewa na;
KATIBU
MKUU
WIZARA
YA NISHATI NA MADINI
9/2/2017
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...