Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Msanii wa Bongo fleva Khalid Mohamed (TID) amesema kuwa hawezi kufumbia macho wala kuwaonea aibu kwa kuwataja watu wote ambao wanafanya biashara ya dawa za kulevya.

TID amesema hayo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa mkuu wa mkoa na waandishi wa habari juu ya mapmbano dhidi ya dawa za kulevya kwa mara ya tatu.

“Mimi mnyama na mkuu wa mkoa kaonesha unyama katika kupambana na madawa ya kulevya, hivyo namshukuru sana kwa hatua ngumu aliyoamua kuichukua,basi wote kwa pamoja tuanze kupambana na kuhakikisha biasha hii inapungua kama sio kuisha kabisa,tushiriki kwa pamoja kukomesha biashara hii kwa kupinga janga hili ” amesema TID.

TID ambaye amekiri hadharani kuwa amekuwa akitumia dawa za kulevya kwa muda mrefu lakini zimekuwa zikimtesa ,hivyo RC Makonda amekuwa msaada kwake,akasema na kuongeza kuwa hahitaji nguvu ya dola kuacha uvutaji wa dawa za kulevya,hivyo ameamua kuacha mwenyewe ili awe mfano wa kuigwa .

Amesema yeye bado ni kijana hana kasoro yoyote wala ulemavu wowote,hivyo itakuwa ni aibu kwake kuonekana mtumiaji wa dawa za kulevya mbele ya mtoto wake, hivyo atakuwa hajengi familia bali atakuwa anaibomoa kwa kumfanya mtoto aendelee kuiga tabia mbovu za baba yake. 
TID ambaye aliiongea kwa ujasiri mkubwa bila kuhofu lolote akiwaomba Watanzania wamuelewe na kumpokea tena,kama kijana aliye amua kuacha matumizi ya dawa za kulevya. 
TID akikumbatiwa na Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Rogers Sianga mara baada ya kumaliza kuzungumza wazi na kukiri kuwa ni kweli alikuwa anatumia Dawa za Kulevya na sasa ameweka wazi kuwa ameacha na yuko tayari kutoa ushirikiano katika suala zima la kupamba na dawa za kulevya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...