Gavana wa Jimbo Katanga Jean Claude Kazembe amesema kuwa ili urahishaji wa ujenzi wa daraja katika mto Lwapula uliopo katika mpaka wa Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) utasaidia kurahisha usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya Dar es salaam kwenda Jimbo la Hault Katanga DRC.

Gavana huyo ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya ziara yake katika Badari ya Dar es salaam.

Alisema kuwa endapo nchi za Zambia na DRC zitakubaliana kujenga Daraja hilo, kutaimarisha  biashara pamoja na kukuza uchumi wa nchi za Tanzania, DRC  na Zambia kwa kuwa itachukua muda mfupi kwa Wasafirishaji wa Mizigo kutoka Dar es salaam kwenda DRC.

“Kujengwa kwa daraja hilo kutarahisisha usafirishaji wa mizigo  kutoka nchini Tanzania kwenda nchini DRC, na hivyo kufanya gharama za usafirishaji wa mizigo kupungua” alisema Gavana Kazembe.

Gavana Kazembe aliongeza kuwa daraja hilo litakalogharimu dola milioni 85 litakalikuwa na urefu wa mita 700  linatarajiwa kujengwa kwa ushiririkiano wa Serikali za  nchi za Tanzania, Kongo na Zambia kwa vile litanufaisha nchi hizo kiuchumi.

Aidha, Gavana Kazembe alisema kuwa atajitahidi kushauri Serikali hizo zijenge daraja katika mto Lwapula ili kusaidia Bandari ya Dar es salaam kuendelea kutoa  huduma nzuri za usafirishaji wa mizigo kati ya Dar es Salaam na Kongo.

Aidha, alisema kuwa katika mazungumzo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alifurahishwa na hatua hiyo kwa kuwa  itasaidia kukuza urafiki uliopo baina ya Tanzania na Kongo pamoja na kurahisisha usafirishaji wa mizigo na kwa gharama nafuu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...