Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Serikali chini ya Wizara ya Hbari Utamaduni Sanaa na Michezo inaendelea na juhudi za kuhakikisha kuwa Utamaduni wa Mtanzania unakuwa sehemu ya muhimu ya kivutio cha Utalii ili kutengeneza ajira na kuingizia Serikali mapato.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye alipokuwa anafungwa maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Washirazi yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa madhimisho haya yanaimarisha undugu wa damu wa kiuchumi na kiutamaduni ulioachwa na wahenga.
“Maadhimisho ya wiki ya Utamaduni wa Shirazi ni fursa pekee ya kujifunza kutoka kwa kwa wairani namna ya kukuza ,kulinda na kuendeleza Utamaduni,Sanaa,Filamu,Mila na Desturi zetu”Alisema Waziri Nape.Aidha ameongeza kuwa Wizara yake itaweza kufanikisha shughuli za Utamaduni na kuziendeleza kwa kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya ya nchi kama ilivyofanyika katika maadhimisho ya mwaka huu kwani yanatangaza vikundi vya Sanaa na Wasanii.
Kwa upande wa wake Mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Irani hapa nchini Bw.Ally Baghari amesema kuwa ushirikiano wa Kiutamaduni baina ya Tanzania na Irani umeongeza mafanikio ya kiuchumi na kijamii katika nchi hizo hasa kupitia ubadilishanaji wa Utamaduni tangu enzi za ukoloni.
“Tumejifunza utamaduni wa kitanzania kupitia maadhimisho haya na tunaamini watanzania pia wamejifunza utamaduni wa Irani ambao umesaidia kuimarisha ushirikiano wetu”Alisema Bw Baghari.
Maadhimisho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akicheza Bao na Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Jadi Tanzania Bw. Mohamed Kazingumbe (kulia) wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiangalia moja ya vitabu vyenye maneno ya Kishiraz wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Bibi. Lilian Beleko, Balozi wa Iran nchini Mossa Farharng na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran Ali Bagheri.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akisikiliza maelezo kuhusu michoro ya Kiutamaduni ya Iran wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akipiga Gitaa lililotengenezwa na Msaanii wa Uchoraji na Uchongaji Bw. Washington Steven Masanja (kushoto) wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania jana jijini Dar es Salaam.Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng akimkabidhi zawadi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...