Serikali imesema
itatoa eneo linalomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Buhemba,
Mkoani Mara kwa wachimbaji Wadogo wa Madini baada ya kufanyika kwa tathmini na taratibu za kumilikishwa eneo ili wachimbaji
hao wafanye shughuli hizo kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu ikiwemo
kulipa kodi.
Kauli hiyo imetolewa
na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo leo tarehe 18
Februari,2017, wakati wa ziara yake katika mgodi huo ili kuangalia shughuli za
uokoaji zinazoendelea katika mgodi huo, kufuatia ajali ya kufukiwa na kifusi kwa Wachimbaji 18 iliyotokea tarehe 13 Februari,2017, ambapo
wachimbaji 13 waliokolewa siku hiyo hiyo
Prof. Muhongo amesema kuwa, wachimbaji hao hawakuwa na
leseni wala vibali halali vilivyotolewa kwao
kufanya shughuli za utafutaji dhahabu na kwamba eneo hilo linamilikiwa
kisheria na STAMICO kwa leseni PL N0.
7132/2011, na kuongeza kuwa, wachimbaji hao walivamia eneo hilo ambapo ni kosa
kisheria na wanatambulika kama wavamizi.
Ameongeza kuwa,
shughuli za uchimbaji katika eneo hilo zilifungwa tangu mwaka 1971 ambapo awali
eneo hilo lilikuwa chini ya wakoloni kabla ya kuwa chini ya uangalizi wa
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Kampuni ya
Meremeta na baadaye kuwa chini ya umiliki wa STAMICO.
Aidha, amezuia shughuli
zote za uchimbaji kufanyika katika eneo hilo na kusema kinachofanyika sasa ni
kuutafuta mwili wa mchimbaji mmoja ambaye bado haujatolewa. ''Hadi sasa
wachimbaji 15 wamekwisha okolewa, bahati mbaya wawili walitolewa wamefariki na
sasa tuendelee na zoezi la kutafuta mwili uliobaki,"ameongeza Prof.
Muhongo.
Mmoja wa wachimbaji waliokolewa katika ajali ya kifusi akimweleza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) jinsi ajali hiyo ya kufikiwa na kifusi wachimbaji 18 ilivyotokea. Katikakti anayesikiliza ni Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje.
Mmoja wa wachimbaji wadogo akishuka chini ya shimo la kuingilia katika mgodi kwa ajili ya kusaidia shughuli za uokoaji kufuatia ajali ya kufukiwa na kifusi wachimbaji 18 katika eneo la Buhemba mkoani Mara.
Sehemu ya Wachimbaji wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa ziara yake katika mgodi wa Buhemba unaomilikiwa na STAMICO.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiongea na wachimbaji wadogo katika eneo la Buhemba ambapo ajali ya wachimbaji wadogo walifukiwa na kifusi tarehe 13 Februari,2017.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...