Na Eliphace Marwa, Dar es salaam

Chama cha Wakandarasi Tanzania kimeiomba Serikali kuwashirikisha katika zabuni za ujenzi wa miradi mbalimbali ya umma Wakandarasi wazawa.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Chama hicho, Mhandisi Lawrence Mwakyambiki wakati mkutano na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali katika sekta ya ujenzi hapa nchini.

Alisema kuwa wanaiomba Serikali ya Awamu ya Tano kuwashirikisha wakandarasi wa kitanzania , wakimemo wakandarasi wa madaraja yote ili waweze kujijengea kitaalamu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo ujenzi wa majengo mbalimbali ya Serikali mkoani Dodoma.

Mhandisi Mwakyambiki aliongeza kua hatua hiyo itasaidia kuongeza ajira kwa vijana na Kampuni za kitanzania katika shughuli za ujenzi hapa nchini.

Aidha, Chama hiyo kimeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza mikakati na kusimamia sekta ya ujenzi hapa nchini.

Aidha Mwakyambiki aliongeza kuwa kutokana na uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano kuhamia Dodoma ni vema wakandarasi wa ndani wakapewa fursa ya kushiriki katika kandarasi mbalimbali ambazo serikali inatarajia kuzifanya huko Dodoma.

Kwa upande Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi John Bura alimshukuru Rais Magufuli na Serikali yake kwa kuitikia wito wa wakandarasi kwa kuwatengea miradi michache ambayo ilikwisha tangazwa.

Aliwataka wakandarasi kuunda umoja kwa ajili ya kuitekeleza kwa weledi ili kuongeza imani kwa Serikali. 
Mwenyekiti wa Chama Cha Wakandarasi Tanzania, Mhandisi Lawrence Mwakyambiki akisistiza jambo kwa waandishi wahabari (hawapo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam kuhusu Serikali kuwapa kipaumbele wakandarasi wa ndani katika miradi ya ujenzi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...