SERIKALI imewataka wanahabari kusoma sheria, taratibu na kanuni zinaogusa tasnia yao ili iweze kuendelea na kuachana na kuamini kila kitu wanachoambiwa na mtu mmoja.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye wakati  akizungumza katika siku ya radio duniani, hafla iliyofanyika Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam.

"Watu someni sheria, taratibu na kanuni kwa kina ili kujua na kuzielewa, mkielewa kama kuna sheria inakwaza ukuaji wa sekta ya habari tuseme tukae chini.. " alisema Waziri Nape akijibu hoja kuhusu sheria za habari zilizopo ambazo zinadaiwa kukwaza uhuru wa ukusanyaji wa habari.

Ilielezwa katika hafla hiyo kuwa sheria za sasa ya takwimu na habari  zinakwaza uhuru wa sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Katika hoja hiyo Makamu mwenyekiti wa Umoja wa Redio za Jamii (COMNETA) Prosper Kwigize katika hotuba yake kwa Serikali, alisema kwamba redio hizo zinachangamoto nyingi katika utendaji wake ikiwamo sheria zilizopo,watoa habari wasioeleweka na wanazuia upatikanaji wa habari.

Nape alisema kwamba sheria si msaafu na kwa kuwa asilimia 80 za habari zinazalishwa na serikali, waandishi wanahaki ya kupata habari hizo na kama kuna kikwazo ni lazima kitafutiwe suluhu.

"Tukae tushindane kwa hoja tukubaliane na kuhakikisha kwamba tunarekebisha.. Bunge kazi yake ni kutunga na kufuta sheria" alisema Nape ambaye alisema kwamba sheria ya sasa imetoa nguvu kwa watoa habari na kwamba si kila habari iliyopo serikalini ni classified.
 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye (wa pili kulia) akimpongeza Meneja wa Redio Jamii Orkonerei  FM, Baraka David Ole Maika baada ya kuwasilisha risala ya mafunzo ya ufundi kwa Redio za Jamii  wakati maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria jijini Dar es Salaam jana. Kulia  Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi, Wa tatu kulia ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues, Wanne kulia Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu na Menejementi ya Teknolojia  wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Dr. Edephonce Nfuka na Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Vyombo vya Habari vya Jamii (COMNETA), Prosper Kwigize.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
  Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akisheheresha kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya radio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Zulmira Rodrigues akitoa neno la ukaribisho liliombatana na ujumbe maalum kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...