Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka wanasheria wa mkoa wa
Dar es Salaam kujitoa kwa kuwasaidia wanyonge na masikini kuweza
kupata haki zao na sio kutumia taaluma katika kuwatetea watu wanaofanya
uhalifu.
Makonda
ameyasema hayo wakati alipokuwa akipokea mrejesho kwa wanasheria
waliojitolea kutoa msaada wa kisheria kwa jiji la Dar es Salaam, amesema
kuwa kuna watu wanakosa haki kutokana na kukosa msaada wa kisheria.
Amesema
kuwa wanasheria wa mkoa wa Dar es Salaam wakijitoa watakuwa wamesaidia
wananchi kupata haki pamoja na kupunguza migogoro iliyopo.
Makonda amesema vijana waliotoa msaada wa kisheria wameonyesha uzalendo na kuwataka kuendelea kuwatumikia wananchi.
Mwakilishi
wa Wanasheria waliojitolea kutoa msaada wa Kisheria, Georgia Kamina
amesema kuwa wamesaidia makundi mengi ikiwa ni pamoja na kukutana na
wananchi.
Georgia amesema walichojifunza katika kazi walioifanya ni wananchi kushindwa kujua sheria na jinsi ya kupata haki.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa
habari juu umuhimu wanasheria kujitoa kwa ajili ya kuwatetea wanyonge jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwakilishi wa Wanasheria
waliojitolea kutoa msaada wa Kisheria, Georgia Kamina.Picha na
Emmanuel Massaka,Globu yaj jami.
Mwakilishi
wa Wanasheria waliojitolea kutoa msaada wa Kisheria, Georgia Kamina
akizungumza na waandishi wa habari juu msaada wa sheria walitoa kwa
wananchi wa Jiji la Dar es Salaam, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda.
Sehemu ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...